• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na rais wa Gabon

    (GMT+08:00) 2018-01-16 20:55:45

    Rais Ali Ben Bongo wa Gabon amekutana na Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ikulu mjini Libreville.

    Rais Bongo amesema Gabon ina rasilimali nyingi na nguvu kubwa za kiuchumi ambazo hazijatumiwa ipasavyo, na kuongeza kuwa nchi yake imeandaa mkakati anuwai wa uchumi na kutumai China itakuwa mwenzi wa ushirikiano anayetegemewa zaidi, na kushiriki kwenye mchakato wa maendeleo ya Gabon katika sekta ya madini, uvuvi, na kilimo. Amesema Gabon ina nia ya kushiriki katika ujenzi wa pamoja wa "Njia Moja, Ukanda Mmoja", na kutoa mchango kwa mkutano wa Baraza la Ushiriano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mjini Beijing.

    Kwa upande wake, Bw. Wang Yi amesema uhusiano wa China na Gabon ni wa ushirikiano wa kiwenzi wa pande zote, na China inapenda kushirikiana na Gabon kufinikisha mkutano wa FOCAC utakaofanyika Beijing na kuendeleza uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Afrika kwa kupitia kujenga kwa pamoja "Njia Moja na Ukanda Mmoja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako