• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Rwanda asema Rwanda itazingatia zaidi mafungamano ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-17 09:23:58

    Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema Rwanda ikiwa nchi inayotarajiwa kuwa mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, itazingatia zaidi mafungamano ya kiuchumi barani Afrika.

    Amesema mchakato huo utawawezesha waafrika kufanya biashara, kuwekeza na kushirikiana na nchi nyingine duniani.

    Rais Kagame amesema sera mpya ya viza ya Rwanda ni moja kati ya hatua za kuhimiza mafungamano, na kusema Rwanda imefungua mipaka yake kwa watalii kutoka nchi mbalimbali duniani ambao wanaweza kupata viza wanapowasili nchini humo.

    Pia amesisitiza kuwa kufungua mipaka kunahitaji nchi yake iwe na tahadhari zaidi, na kuanzisha mifumo ambayo ina ufanisi zaidi. Rais Kagame anayeongoza mchakato wa mageuzi ya Umoja wa Afrika, pia amesema mageuzi ya kitaasisi na kifedha bado yanaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako