• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga, Chama cha raga Kenya kuvunja mikataba na wachezaji kutokana na ukata.

    (GMT+08:00) 2018-01-17 11:17:14

    Wasiwasi umetanda baada ya chama cha raga cha nchini Kenya, KRU kutangaza kuwa, huenda kikavunja mkataba baina yake na wachezaji pamoja na benchi zima la ufundi.

    Mwenyekiti wa KRU Richard Omwela amesema kuwa, wamelazimika kukata mishara ya malipo mengine ya mwezi kutokana na uhaba wa fedha baada ya wadhamini wao wakuu kampuni ya sportpesa kujitoa.

    Kabla ya sportpesa kujitoa, pande hizo mbili mwaka 2016 zilisaini mkataba wa ufadhili wa miaka mitano, wenye thamani ya shilingi milioni 607 uliokuwa na fungu la milioni 60 kila mwaka lililokuwa likitumiwa na timu za taifa za wanaume, wanawake na timu za vijana.

    Na yote haya yanakuja wakati ambapo leo hii kocha mkuu wa timu ya taifa Innocent Simiyu alitarajiwa kutaja kikosi kitakachoshiriki mashindano ya chama cha raga duniani dhidi ya Australia na New Zealand januari 26 na januari 28.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako