• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Rayon Sports yamsajili Yassin Mugume wa Uganda

    (GMT+08:00) 2018-01-17 11:19:45
    Ili kujiimarisha kwenye ligi kuu inayeondelea nchini Rwanda, klabu ya Rayon Sport imekamilisha usajili wa mshambuliaji Yassin Mugume kutoka timu ya Polisi FC inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda.

    Nyota huyo mwenye miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya faranga za Rwanda milioni 6, na atakuwa akilipwa mshahara wa faranga 400,000 kwa mwezi.

    Taarifa zinasema kuwa, endapo Yassin Mugume atafanya vizuri basi mkataba wake na Rayon unaweza kuongezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako