• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika kuwa wenzi wa karibu zaidi kwenye ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2018-01-17 18:59:58

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amemaliza ziara yake katika nchi nne za Afrika na kusema, China na Afrika zitakuwa wenzi wa karibu zaidi kwenye ujenzi wa pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Bw. Wang amesema, desturi ya waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara ya kwanza ya kila mwaka barani Afrika imedumu kwa miaka 28. Desturi hiyo imethibitisha kuwa bila kujali jinsi China inavyoendelea, inajichukulia kama nchi inayoendelea. Amesema China na nchi za Afrika zinaweza kuwa wenzi wa kuaminiana na kushirikiana kwenye sekta za uchumi na siasa.

    Akizungumzia ziara hiyo, Bw. Wang amesema, ushawishi wa kimataifa wa mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC bado unaendelea kuenea hasa kwenye nchi zinazoendelea. Nchi mbalimbali za Afrika zinataka kufuata mkakati anuwai wa uchumi, na pia kuimarisha ushirkiano na China, hivyo mkutano wa kilele wa FOCAC utakaofanyika hapa Beijing mwaka huu utakuwa mkutano wa kihistoria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako