• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Olimpiki, Timu za Korea ya Kaskazini na Korea Kusini zapendekeza kuungana wakati wa mashindano ya Olimpiki.

    (GMT+08:00) 2018-01-18 08:14:20

    Kwa kile kinachoweza kuitwa ni historia ya kipekee duniani, timu za Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini zimekubaliana kuungana wakati wa hafla ya ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki katika majira ya baridi ambapo wachezaji wa mataifa hayo mawili watavaa sare zinazofanana, na wataingia kwenye gwaride la ufunguzi chini ya bendera moja ya muungano wao kuuthibitishia ulimwengu kuwa mazungumzo yao ya maelewano yamefana.

    Aidha timu hizo zimekubaliana kuunda timu ya pamoja ya wanawake ya mchezo wa mpira wa magongo ya kuteleza kwenye barafu, na ili kuongeza hamasa Korea Kaskazini itatuma mashabiki 230 kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika mjini PyeongChang nchini korea Kusini.

    Hata hivyo hayo ni maamuzi ya mkutano wa majadiliano uliotoa mapendekezo hayo ambayo juma lijalo utayawasilisha kwenye kamati ya kimataifa ya Olimpiki ili kuomba ridhaa ya kufanya hivyo siku ya ufunguzi wa mashindano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako