• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika watoa wito kwa wanawake wa Afrika kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ufisadi

    (GMT+08:00) 2018-01-18 09:07:11

    Mkutano wa 10 wa Umoja wa Afrika unaohusu mambo ya kijinsia umefanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia na kutoa wito kwa wanawake barani Afrika kujiunga kwenye mapambano dhidi ya ufisadi.

    Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia mambo ya kisiasa Bibi Minata Cessouma amesema, mkutano huo ni muhimu katika kushawishi sera za umoja huo za usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake. Pia umetoa fursa kupitia maendeleo yaliyopatikana katika miaka 10 iliyopita, na kupanga kazi za siku za baadaye hasa katika mageuzi ya umoja huo na ajenda ya kuelekea mwaka 2063.

    Bibi Cessouma amesema, ufisadi ni kikwazo kikubwa zaidi katika kutimiza ajenda ya 2063, na mkutano huo utasaidia umoja huo kuendeleza mikakati mpya ya kupambana na ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako