• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasomi kutoka Afrika, wakipongeza chama cha CPC kwa kutoa muongozo kivitendo wa namna ya kupunguza umaskini duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-18 19:38:39

    Washiriki wa semina maalum kuhusu zama mpya za maendeleo ya uchina na fursa mpya katika ushirikiano wa China na Afrika ambayo kwa kiasi kikubwa imelenga kubadilishana uzoefu katika kupambana na umaskini pamoja na kujadili kwa pamoja namna bora za kupambana na umaskini wameipongeza serikali ya China chini ya chama cha CPC kwa kufanikiwa kupunguza umaskini kupitia utekelezaji wa kivitendo na kwa wakati sera zilizowekwa, lakini kwa kutoa mwelekeo sahihi wa kupambana na umaskini.

    Idhaa ya Kiswahili ya redio China kimataifa imefanikiwa kuzungumza na baadhi ya washiriki ambao ni wasomi kutoka nchi za Afrika mashariki, ambapo licha ya kueleza ufahamu wao juu ya maendeleo ya China katika kupambana na umaskini, pia wameweka wazi tofauti kubwa iliyopo katika njia za kupambana na umaskini kati ya China nan chi nyingine duniani, hivyo wakitoa ushauri kwa nchi za Afrika kuhusu mambo ya kujifunza kupitia ushirikiano wa China na Afrika.

    Walter Bgoya yeye ni mkurugenzi wa kampuni ya uchapishaji wa vitabu nchini Tanzania, yeye amezitaka nchi za Afrika kubadili mtazamo wake wa namna ya uongozi wa nchi, akizitaka kutotumia vibaya fursa iliyotolewa na China ya kupata maendeleo kupitia usimamizi thabiti wa misingi iliyowekwa.

    WALTER BGOYA

    "mimi nadhani sasa tukubaliane kwamba magharibi sasa haitupi mfano wowote, ubepari hautupi mfano wowote wa mafanikio, tuemajaribu ubepari miaka yote hiyo, tumeishindwa. Ambazo zimeshinda ni zile amabzo zimechukua mithili ya China, mfano wake ni uongozi wa namna hii, mifano iko hapa China na katika semina hii tunajifunza, wanavyopambana na umaskini kutoka ngazi za juu hadi chini, hadi kuisaidia familia kuiondoa katika umaskini, na kuishirikisha katika mipango na miradi ya kuondokana na umaskini, wanaofanya ni nani, Viongozi wa chama, na viongozi wa serikali na viongozi wa ngazi za chini, halafu mipango, wana mpango wa taifa na hata mpango wa ngazi ya mkoa.

    "

    Kwa upande wake Profesa Kenneth Inyani Simala kutoka baraza la Kiswahili la nchi za Afrika Mashariki, amezungumzia namna ambavyo ushirikiano baina ya China na Afrika unaweza kuimarishwa kwa lengo la kupata maenedeleo kwa pamoja akitolea mfano mabadilishano ya utamaduni.

    PROFESSOR KENNETH SIMALA

    "kwa hiyo tusiufunge ushirikiano baina ya China na Afrika kwa kiwango cha kitaifa pekee, tuuweke pale chini, na nitatoa mfano wa Afrika Mashariki, ushirikiano unaweza kujengwa vizuri sana katika misingi ya utamaduni, hivi sasa wachina wanaendelea na kitu ambacho wanazingatia ni utamaduni wao, na kuna rasilimali kubwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ni lugha ya Kiswahili, kwa nini wachina wanajifunza lugha ya kiswahili, wanatambua kuwa ili wafanikiwe katika miradi wanayoiendeleza katika jumuiya ya Afrika Mashariki hawana budi kujifunza kiswahili, hivyo ushirikiano baina ya wanataaluma wa Chinana Afrika Mashariki unahitajika kwa sababu lugha ndiyo nembo na Kitovu cha kuwafanya watu waelewe maendeleo."

    Naye Profesa Gideon Munene kutoka Chuo Kikuu cha Kimarekani cha jijini Nairobi, amekumbusha umuhimu wa nidhamu pamoja na unyenyekevu wakati wote katika kutekeleza maazimio ili kufikia malengo ya maendeleo, akisema hilo ni jambo muhimu la kujifunza.

    PROFESSOR GIDEON MUNENE

    "Uongozi wa Uchina una huo mwelekeo, nia nzuri ambayo ni kamilifu, na wanajua nini wanafanya, na kuna jambo linguine ambalo China inaonekana iko mbele ya zingine, ile unyenyekevu katika siasa za duniani, sio kujigamba kila wakati hata kama wanaonekana wameenda mbele, tumetembea tembea tumeona mambo yamefanyika hapa China ni mambo ya juu zaidi, na hata siku moja huwezi kuta wanajitangaza kwamba wako mbele, lakini utawasikia wakisema tungalibado tunaendelea ili kufikia kiwango fulani, tunatarajia kufika lakini bado hatujafika, kule kukubali, maana kuna watu wengi walitamani kufika kiwango hicho kasha wajigambe, na hiyo ni nguvu."

    Na Profesa AIdin Mutembei kutoka idara ya mafunzo ya ushirikiano baina ya China na Tanzania (Confucius Institute) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, ambapo yeye ameelezea mambo muhimu ya kujifunza akitolea mfano umuhimu wa kuwa na mtazamo wa pamoja katika kufanikisha maendeleo akitolea mfano, mapendekezo ya mkutano mkuu wa 19 wa CPC.

    PROFESSOR ALDIN MUTEMBEI

    "mkutano wa 19 wa CPC, kitu ambacho nimejifunza, ni jinsi ambavyo chama kinatoa mwelekeo, chama kinatoa maelengo kwamba tunataka twende sehemu Fulani, na kila mtu katika chama, au serikali na yeyote yule katika shule, biashara anazungumza akiwa na lengo hilo, kwa hiyo kila mtu atafute nafasi yake, kwamba mimi nafanya biashara, je nitafanyaje biashara katika kuelekea lengo hilo, mimi ni mwalimu wa historia hivyo nitafanyeje katika kuwaelekeza wanafunzi wangu kuelekea katika lengo hilo, hivyo chama kinafanya vizuri kina ushusiano mkubwa na serikali na kila mtu hakuna cha chuki na siasa, na ni lazima turudishe ilivyokuwa mwanzo, kwamba cham kinatoa mwelekeo na kila mtu anafuata, na kama kuna mtu anapingamizi basi anatoa ushauri mbadala kuboresha bila kupinga ili kufikia lile lile lengo moja."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako