• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Bei ya mafuta yasalia juu

    (GMT+08:00) 2018-01-18 19:58:09

    Mamlaka ya kudhibiti bei nchini Rwanda (RURA) imetangaza kuwa bei ya mafuta itasalia Rwf970 kutoka Rwf 932 kwa lita kufuatia msimamo wa bei ya kimataifa ya mafuta.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na RURA, Meja Jenerali Patrick Nyirishema amesema kuwa bei mpya ya mafuta iliyotumika wiki jana itaendelea kusalia hadi pale kutakapokuwa na mabadiliko.

    Hii inamaanisha kuwa bei ya petrol imeongezeka kwa Rwf22 na diesel Rwf 18 kwa lita.

    Nchi wanachama wa uzalishaji mafuta OPEC zilikubaliana kuendelea na kupunguza bidhaa hiyo sokoni kwa mda .

    Kuanzoa mwisho wa mwaka 2016 nchi hizo zilikubaliana kuuza mapipa milioni 1.8 pekee kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako