• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Bodi ya kahawa yasaka wateja zaidi

    (GMT+08:00) 2018-01-18 19:59:52

    Halmashauri ya kahawa nchini Uganda inaazimia kufikisha mauzo ya magunia milioni 20 ya kahawa katika nchi za nje.

    Uganda itashirikiana na zaidi ya mashirika 40 kujadiliana na kuweka mbinu za kupanua mauzo yao.

    Miradi 9 ya kufikisha bidhaa hiyo katika nchi za nje imeanzishwa ikilenga kuboresha uzalishaji na kukabiliana na changamoto za biashara hiyo.

    Kwa mujibu wa Emmanuel Niyibigira ,meneja wa halmashauri ya maendeleo ya kahawa Uganda,agizo la kufikisha mauzo ya magunia milioni 20 kufikia mwaka 2025 linawezekana bila mushkil.

    Kuingia kwa muungano wa EU katika ushirikiano na Uganda kwenye lengo hilo,kumetatua utata wa fedha uliokwamisha maendeleo.

    Aidha kampuni za utayarishaji na wakulima wametakiwa kuboresha kahawa wanayozalisha ili ipenye kwenye soko la kimataifa.

    Uganda ina asilimia 6 tu ya wateja wa jahawa idadi ambayo bodi ya kahawa haijaridhishwa nayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako