• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwanja mpya wa ndege wa Beijing kufanyiwa majaribio mwezi Oktoba mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-01-19 08:45:44

    Uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Beijing utaanza kufanyiwa majaribio mwezi Oktoba mwaka 2019. Ofisi ya manispaa ya Beijing inayoshughulikia uratibu na uhimizaji wa ujenzi wa uwanja huo, imesema miradi ya uhandisi itakamilika mwezi Julai mwaka kesho, huduma za majaribio zitaanza miezi mitatu baadaye. Uwanja huo mpya ulioko kilomita 46 kusini mwa mji wa Beijing, umesanifiwa kupunguza shinikizo kwa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing, na utakuwa na uwezo wa kushughulikia safari laki 6.2 za ndege kila mwaka na kupokea abiria milioni 100 na tani milioni 4 za mizigo kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako