• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi 95 wa misaada wauawa nchini Sudan Kusini ndani ya miaka minne

    (GMT+08:00) 2018-01-19 09:03:30

    Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA, imesema wafanyakazi 95 wa misaada wameuawa tangu kutokea kwa mgogoro wa Sudan Kusini mwezi wa Desemba mwaka 2013.

    OCHA imesema, mwaka jana matukio 1,159 ya kushambuliwa kwa watoa misaada ya kibinadamu yaliripotiwa, yakiwemo ya mauaji, unyang'anyi, ujambazi, tishio na usumbufu. Idadi hiyo imeongezeka kwa kasi ikilinganishwa na matukio 908 ya mwaka 2016, na 909 ya mwaka 2015. OCHA imesema, matukio hayo yaliiathiri zaidi miji ya Juba, Rubkona na Wau.

    Pia imesema zaidi ya nusu ya wafanyakazi 612 walioshambuliwa na kuhamishiwa kwenda miji mingine katika mwaka jana, waliishi Koch, Leer, Mayendit na Akobo, ambako watu laki 5 wanahitaji misaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako