• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapiga marufuku utengenezaji na mauzo ya pembe za ndovu

    (GMT+08:00) 2018-01-19 10:05:20

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amekumbusha kuwa China imepiga marufuku utengenezaji na mauzo ya bidhaa za pembe za ndovu. Msemaji huyo amesema Idara ya Misitu ya China ilitangaza marufuku hiyo mwishoni mwa mwaka jana. Hadi sasa viwanda 34 vya utengenezaji na vituo 143 vya mauzo vimefungwa nchini China.

    Bw. Lu Kang amesema, hatua hiyo imepongezwa na nchi nyingi za Afrika, kwa kuwa inasaidia kukata mnyororo wa biashara ya pembe za ndovu kutoka kwenye chanzo chake, kulinda tembo wa Afrika na mfumo wa ikolojia barani Afrika na hata dunia nzima, na kufunga soko kubwa la biashara ya pembe za ndovu duniani.

    China ikiwa nchi iliyosaini Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Mimea na Wanyama walio hatarini, imekuwa ikitimiza majukumu yake, na imetoa mchango mpya katika kulinda wanyamapori barani Afrika kutokana na kupiga marufuku biashara ya pembe za ndovu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako