• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Somalia vyatwaa mji wa kusini wa Bar-Sanguni

    (GMT+08:00) 2018-01-19 10:08:22

    Jeshi la Somalia limeukomboa mji wa kusini wa Bar-Sanguni kutoka kwa kundi la Al-Shabaab, na kuwaua wapiganaji saba wa kundi hilo, wakiwemo maofisa wake wanne waandamizi.

    Kamanda mkuu wa divisheni ya 43 ya jeshi la Somalia iliyoshiriki kwenye operesheni hiyo Jenerali Ismail Sahardid hakutaja idadi ya majeruhi kwa jeshi lake kwenye operesheni hiyo, na kuongeza kuwa jeshi lake limewakamata mafundi wawili kutoka kwa kundi la IS.

    Jeshi la Somalia limeimarisha operesheni zake kutoka angani na ardhini dhidi ya Al Shabaab, kufuatia mpito wa kuondoa vikosi vya Umoja wa Afrika kulingana na mazingira ya usalama kuanza kutekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako