• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wagundua mlipuko mkubwa zaidi wa volkeno chini ya bahari

    (GMT+08:00) 2018-01-19 15:11:40

    Wakati wanasayansi wa Australia walipochambua mwamba unaoelea baharini, wamegundua kuwa mlipuko wa volkeno ya Havre iliyoko karibu na New Zealand uliotokea mwaka 2012 ni mlipuko mkubwa zaidi wa volkeno kutokea chini ya bahari.

    Mtaalamu wa volkeno wa Chuo kikuu cha Tasmania Rebecca Carey na wenzake hivi karibuni walitoa ripoti kwenye gazeti la Science Advances la Marekani ikisema waligundua mwamba unaoelea baharini wenye ukubwa wa kilomita 400 za mraba kwenye bahari karibu na New Zealand kupitia satilaiti mwaka 2012, na uchambuzi unaonesha kuwa mwamba huo unaundwa kwenye mlipuko wa volkeno ya Havre iliyoko kilomita 1000 kutoka kisiwa cha kaskazini cha New Zealand.

    Mwaka 2015, watafiti walianza kupima, kuchunguza na kukusanya sampuli za volkeno ya Havre kwa vyombo vinavyosafiri chini ya maji, na kugundua kuwa mlipuko wa volkeno hiyo katika mwaka 2012 ni mlipuko mkubwa zaidi wa volkeno chini ya bahari katika miaka 100 iliyopita. Kwenye mlipuko huo, lava zilitoka sehemu 14, hii inamaanisha kuwa volkeno ilivunjika katika sehemu nyingi.

    Watafiti pia wamesema asilimia 80 ya volkeno duniani ipo chini ya bahari, hivyo kuelewa milipuko ya volkeno chini ya bahari ni kazi muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako