• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Dinosaur mwenye manyoya ya rangi za upinde wa mvua agunduliwa nchini China

  (GMT+08:00) 2018-01-19 15:15:10

  Kisukuku cha dinosaur mwenye manyoya cha mwishoni mwa enzi ya Jurassic kimegunduliwa mkoani Hebei, China. Kisukuku hiki kinaonesha kuwa manyoya yanayotofautiana kwenye pande mbili za kushoto na kulia ambayo ni muhimu sana kwa kuruka yalitokea miaka milioni 160 iliyopita, ambayo ni mapema zaidi kuliko kisukuku kilichogunduliwa zamani ambacho ni cha miaka milioni 10.

  Watafiti wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Shenyang na idara ya wanyama wenye uti wa mgongo na binadamu wa kale ya taasisi ya sayansi ya China wametafiti kwa miaka miwili, na kugundua kuwa hiki ni kisukuku cha dinosaur mpya mwenye uhusiano wa karibu na ndege, na kumpa jina la "Caihong Juji" ambalo linamaanisha dinosar "rangi za upinde wa mvua na kishungi kikubwa" kwa sababu wamekisia kuwa ana manyoya ya rangi mbalimbali kama upinde wa mvua.

  Prof. Hu Dongyu wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Shenyang alifahamisha kuwa manyoya yanayotofautiana kwenye pande mbili za kushoto na kulia ni dalili ya upekee wa ndege wa kisasa wanaoruka. Manyoya yanatofautiana kwenye pande mbili za mkia wa dinosaur huyu, na hali hii inaonesha kuwa huenda alikuwa na uwezo wa kuruka, lakini manyoya kwenye mabawa yake mawili bado ni sawasawa, hii inamaanisha kuwa manyoya yanayotofautiana huenda yalitokea kwanza kwenye mkia, na mkia ni chanzo kikuu cha uwezo wa kuruka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako