• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China umekuwa tulivu katika sekta mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-01-19 17:27:18

    Wataalamu wamesema uchumi wa China umekuwa tulivu katika sekta mbalimbali, ikiwemo soko la ajira, bei ya bidhaa na mapato na matumizi ya kimataifa.

    Takwimu zilizotolewa na serikali ya Chinazinaonesha kuwa, pato la taifa la China GDP liliongezeka kwa asilimia 6.9 mwaka jana, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa China kuongezeka baada ya mwaka 2011, mfumuko wa bei ulikuwa katika asilimia 1.6, watu zaidi ya milioni 13 katika maeneo ya mijini na vijijini wamepata nafasi za ajira, na akiba ya fedha za kigeni imefikia dola za kimarekani trilioni 3.14.

    Wataalamu wamesema muundo wa uchumi wa China unaboreshwa, mabadiliko ya nguvu za kukuza uchumi na ubora unaongezeka na kuchangia injini za maendeleo katika muda mrefu na wa kati kwa uchumi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako