• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yawatanga wasagaji wa unga wa mahindi kutoongeza bei

    (GMT+08:00) 2018-01-19 19:08:44

    Serikali ya Kenya imewaonya wasagaji wa unga wa mahindi dhidi ya kuuza bidhaa hiyo kwa zaidi ya shilingi 115 kwa pakiti ya kilo mbili. Waziri wa kilimo wa Kenya Bw William Bett amesema serikali itawachukulia hatua watengenezaji wa unga watakaouza bidhaa hiyo zaidi ya bei iliyowekwa na serikali.Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Bett pia alichukua fursa hiyo kuitetea serikali kuhusiana na uhaba wa mahindi.Hali hiyo imesababbisha bei ya unga wa mahindi kupanda baada ya mradi wa serikali wa unga ya bei ya chini kukamilika mwishoni mwa mwaka jana.Bett amesema wizara yake itahakikisha kuwa bei ya mahindi imekuwa thabiti. Mapema wiki hii, wasagaji walisema bei ya unga wa mahindi kwa pakiti ya kilo mbili ingepanda hadi shilingi 200 kufikia mwishoni mwa machi.Hata hivyo Bett amesema kiasi cha mahindi yaliyopo nchini Kenya kinatosha mpaka msimu unaofuata wa kuvuna zao hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako