• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yaanza operesheni ya kijeshi kaskazini mwa Syria

    (GMT+08:00) 2018-01-22 09:54:01

    Waziri mkuu wa Uturuki Bw. Binali Yildirim ametangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limeingia nchini Syria, na kuanza operesheni ya kijeshi dhidi ya mji wa Afrin, kaskazini mwa Syria.

    Bw. Yildirim amesema lengo la operesheni hiyo ni kuanzisha eneo salama kwenye sehemu ya Afrin, na kwamba magaidi ndio wanaolengwa kwenye operesheni hiyo na wala sio raia, na haitaathiri mchakato wa amani wa Astana unaohusu suala la Syria na mkutano wa viongozi wa Sochi.

    Habari nyingine zinasema mji wa Reyhanli wa Uturuki ulioko mpakani kati ya Uturuki na Syria ulishambuliwa kwa makombora na kusababisha kifo cha mtu mmoja, na wengine 32 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako