• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gorge Weah aapishwa kuwa rais mpya wa Liberia

    (GMT+08:00) 2018-01-23 10:38:25

    Bw. George Weah ameapishwa rasmi kuwa Rais wa Liberia na kuaahidi kufufua uchumi na kupambana na ufisadi.

    Bw Weah aliyekuwa nyota wa soka aliapishwa katika Uwanja wa Samuel Kanyon Doe karibu na Monrovia, mji mkuu wa nchi hiyo.

    Ameahidi kuwa Liberia itakuwa wazi kwa biashara wakati wote, na serikali mpya itaweka mazingira mazuri kwa uwekezaji mkubwa. Pia ameahidi kuwa serikali itawekeza katika sekta za kilimo na miundombinu ili kuboresha maisha ya Waliberia.

    Katika hotuba yake, rais Weah pia amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China moja, na kuahidi kuimarisha uhusiano na China. Pia ameishukuru China na jumuiya ya kimataifa kwa mchango wake kwa Liberia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako