• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya uzalishaji wa mali baharini nchini China kwa mwaka jana yafikia dola trilioni 1.2 za kimarekani

    (GMT+08:00) 2018-01-23 19:12:52

    Takwimu zinaonesha kuwa mwaka jana thamani ya uzalishaji wa mali baharini nchini China ilifikia renminbi yuan trilioni 7.8, sawa na dola trilioni 1.2 za kimarekani. China imepiga hatua kubwa katika shughuli nyingi muhimu za bahari, huku ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitajika kutatuliwa.

    Mwaka jana China ilipiga hatua kubwa katika shughuli nyingi muhimu za bahari, na kutimiza malengo kadhaa kwa mara ya kwanza. Mkuu wa idara kuu ya bahari ya China Bw. Wang Hong amesema, mwaka jana kwa mara ya kwanza China ilifanya usimamizi kwa bahari kama ilivyopangwa ili kuimarisha udhibiti kwa maeneo ya bahari, na pia kwa mara ya kwanza ilifanya uchunguzi kwa mabomba yote ya kutoa uchafuzi kwa bahari, ili kushughulikia uchafuzi wa bahari kwa hatua madhubuti zaidi. Mwaka jana, thamani ya uzalishaji mali baharini nchini China ilifikia yuan trilioni 7.8, ambazo ni asilimia 10 ya thamani yote ya uzalishaji mali nchini China.

    Katika miaka ya hivi karibuni, mageuzi ya shughuli za bahari yamechangia ukuaji wa uchumi wa baharini. Bw. Wang amesema, mwaka jana shughuli za biashara na huduma zilichukua asilimia zaidi ya 54 ya thamani ya uzalishaji wa mali baharini, huku shughuli mpya zinazostawi katika miaka ya hivi karibuni zikiongezeka kwa asilimia zaidi ya 12. Profesa Liu Fang kutoka taasisi ya utafiti wa kimkakati ya idara kuu ya bahari ya China anasema,

    "Kwa mfano utengenezaji wa dawa za viumbe wa bahari ambao ni moja ya shughuli mpya zinazostawi katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya maji baharini, nishati baharini yanayoweza kurudia kutumiwa, vifaa vya utoaji wa mafuta baharini, zikiwemo meli maarufu za Jiaolong na Lanjing No.1, zote ni uthibitisho wa maendeleo ya uchumi wa bahari. Aidha, safari ya meli za anasa za abiria, na huduma za fedha baharini pia zimepata maendeleo makubwa."

    Hata hivyo, China bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika shughuli za bahari. Mwaka huu China itashughulikia suala la kuziba bahari, na kupiga marufuku kitendo chochote cha kuziba bahari kwa ajili ya kujenga nyumba za kibiashara. Aidha, itatoa mpango wa kuhifadhi mistari ya asili ya bahari, na kuweka vigezo mahsusi kwa sehemu zote za pwani. Mbali na hayo, China pia inatakiwa kutatua masuala ya mipangilio inayofanana ya miji pwani, na ugumu wa kubadilisha matokeo ya utafiti wa sayansi kuwa mafanikio ya uchumi. Profesa Liu anasema,

    "Uchumi wetu wa bahari bado una kasoro za kutokuwa na uwiano, uratibu na ukubwa wa kutosha. Aidha, tunapaswa kuboresha mipangilio ya uchumi huo, na kutatua suala la shughuli zinazofanana katika sehemu zote za pwani. Zaidi ya hayo, ni lazima tuongeze kiwango cha kubadilisha matokeo ya utafiti wa sayansi kuwa mafanikio ya uchumi."

    Kuhusu mpango wa muda mrefu, idara kuu ya bahari ya China imekuwa na malengo dhahiri. Hadi kufikia mwaka 2020, China itainua sifa za ongezeko la uchumi wa bahari, na thamani ya uzalishaji wa mali baharini itafikia yuan trilioni 10, na idadi ya watu watakaofanya kazi husika na bahari itafikia milioni 38. Hadi kufikia mwaka 2035, thamani ya uzalishaji wa mali baharini itachukua asilimia 15 ya thamani yote ya uzalishaji mali nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako