• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Paul Kagame awasili Davos, Uswisi kwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia.

    (GMT+08:00) 2018-01-23 19:16:34
    Rais wa Rwanda Paul Kagame amewasili mjini Davos, Uswisi ambako atajiunga na Wakuu wa Nchi na Serikali, pamoja na watendaji wa juu wa kimataifa katika Mkutano wa Mwaka wa 48 wa Uchumi wa Dunia.

    Rais Kagame anatarajiwa kuzungumza katika mkao wa Sera ya Nje ya Washington Post na kutoa hotuba ya mwisho wakati wa kufungwa kwa mkutano wa kujenga amani barani Afrika.

    Mktano wa mwaka huu unaandaliwa chini ya maudhui ya "Kujenga siku za usoni kwa pamoja katika Dunia Iliyovunjika", na utaongozwa na wanawake ambao ni pamoja na; Sharan Burrow, Katibu Mkuu wa Shirika la kimataifa la biashara na Fabiola Gianotti, Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Ulaya la Utafiti wa Nyuklia na Christine Lagarde, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF).

    Mkutano wa mwaka huu umeandaliwa kwa malengo manne muhimu ikiwemo ni kuendesha maendeleo endelevu ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako