• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Awamu ya pili ya mradi wa China wa kutoa matibabu ya saratani ya shingo ya uzazi bila malipo nchini Zimbabwe yazinduliwa

  (GMT+08:00) 2018-01-24 10:32:58

  Awamu ya pili ya mradi wa timu ya madaktari wa China kutoa huduma za upimaji na matibabu ya saratani ya shingo ya uzazi bila malipo nchini Zimbabwe, ilianzishwa Jumatatu wiki hii. Timu hiyo yenye madaktari 10 kutoka hospitali ya wanawake na watoto wa mkoa wa Hunan, wanashiriki kwenye kazi hiyo ya wiki tatu katika hospitali ya Parirenyatwa mjini Harare, Zimbabwe.

  Wakati wa shughuli hiyo, madaktari hao watafanya upimaji kwa wagonjwa wapatao 1000 wa Zimbabwe, na kuwafanyia upasuaji baadhi ya wagonjwa. Mbali na hayo, wameizawadia vifaa vya matibabu hospitali hiyo, na kuanzisha mawasiliano na mafunzo ya kimatibabu, ili kusaidia kuboresha hali ya afya ya uzazi ya wanawake wa huko.

  Katika halfa ya uzinduzi wa shughuli hiyo, balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Huang Ping amesema, China ina ushirikiano mkubwa katika sekta mbalimbali na Zimbabwe, shughuli hiyo ikiwa ni sehemu ya Mpango wa China wa kutekeleza miradi 100 inayohusu afya ya wanawake na watoto ambao ulitolewa na rais Xi Jinping wa China, itahimiza zaidi ushirikiano katika sekta ya afya kati ya China na Zimbabwe.

  Takwimu zimeonesha kuwa, saratani ya shingo ya uzazi ni moja kati ya saratani zinazoenea kwa kasi zaidi miongoni mwa wanawake nchini Zimbabwe, na kiasi hicho kimefikia asilimia 33. Nchini Zimbabwe, watu 2,270 wanagunduliwa kuwa na saratani hiyo kila mwaka, na 1,450 kati yao wamepoteza maisha. Lakini asilimia 13 tu ya watu wanakwenda hospitali kufanyiwa upimaji. Waziri wa afya na utoaji wa huduma kwa watoto wa Zimbabwe Bw. David Parirenyatwa amesema, shughuli hiyo inasaidia kuongeza mwamko wa umma kufanyiwa upimaji wa ugonjwa huo, na kupunguza kiwango cha ugonjwa huo.

  Huduma za matibabu na afya ni moja kati ya sekta za ushirikiano kati ya China na Zimbabwe. Katika miaka 20 iliyopita, serikali ya China imeisaidia Zimbabwe kujenga hospitali mbili, kutoa vifaa vya matibabu vyenye thamani ya dola milioni 2.19 za kimarekani, kutuma madaktari na wataalamu 140 kuisaidia Zimbabwe kuinua kiwango chake cha matibabu na afya, na kuboresha maisha ya watu wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako