• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Serikali yabaini wachimba madini wengi Morogoro hawalipi kodi

    (GMT+08:00) 2018-01-24 19:20:51
    Serikali ya Tanzania aimebaini kuwa baadhi ya wamiliki wa migodi ya madini katika wilaya mbalimbali za Morogoro wanakwepa kodi.

    Utafiti uliofanywa mkoani Morogoro umeonyesha uwapo wa wachimbaji zaidi ya 3,000 lakini kati ya hao ni 76 waliosajiliwa na kati ya hao ni wanne tu wanaolipa kodi na hivyo kuifanya serikali kupoteza mamilioni ya kodi kupitia sekta ya madini.

    Akizungumza katika mkutano maalum wa wadau wa madini ulioratibiwa na Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake(TAWOMA) jana,chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa la Best Dialogue,Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Stephen Kebwe alisema aserikali itaanza kuwaelimisha wenye migodi umuhimu wa kulipa kodi.

    Mkuu huyo wa mkoa alisema endapo hakutakuwa na utekelezaji ulipaji kodi,watendaji wa halmashauri za wilaya husika watasimamia shughuli hiyo ili mamlaka ya mapato (TRA) ikusanye kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako