• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Russia na Uturuki wasisitiza kuendelea kushirikiana kusaidia kutatua mgogoro wa Syria

    (GMT+08:00) 2018-01-24 19:35:27

    Rais Vladmir Putin wa Russia na mwenzake Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wamejadiliana kwa njia ya simu kuhusu hali ya Syria, na kusema wataendelea kushirikiana kusaidia kutatua mgogoro unaoendelea nchini humo.

    Habari zilizotolewa na ikulu ya Russia zimesema, marais hao wamezungumzia operesheni ya kijeshi iliyofanywa na Uturuki mjini Afrin, kaskazini mwa Syria. Pande hizo mbili zimesisitiza ni lazima kuhakikisha ukamilifu wa ardhi na kuheshimu uhuru wa Syria katika utatuzi wa suala hilo.

    Viongozi hao pia wamejadiliana kuhusu maandalizi ya mkutano ujao wa mazungumzo ya taifa ya Syria mjini Sochi, Russia. Pande hizo mbili pia zinatarajia mkutano huo utafikia makubaliano na kupata utatuzi wa kisiasa na wa muda mrefu wa suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako