• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yatangaza mwamuzi wa mechi ya Azam na Yanga

    (GMT+08:00) 2018-01-25 09:25:56
    Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania, TFF limetegua kitendawili kuwa mwamuzi gani atachezesha mechi baina ya miamba ya soka ya nchini humo Azam fc na Yanga itakayopigwa jumamosi ijayo mjini Dar es Salaam.

    Mwamuzi wa kati atakuwa Isreal Nkongo, atakayesaidiwa washika vibendera Josephat Bulali na Soud Lila, mwamuzi wa akiba atakuwa Elly Sasii na Kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir.

    Yanga inazidiwa pointi tano na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya vinara, Simba SC wenye pointi 32.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako