Ofisa mwandamizi wa China Bw. Liu He amefafanua mpango wa ngazi ya juu wa China kuhusu sera za uchumi kwa miaka kadhaa ijayo kwenye mkutano wa Baraza la Uchumi Duniani WEF unaoendelea huko Davos, nchini Uswisi.
Katika hotuba yake Bw. Liu amesisitiza umuhimu kuhakikisha uchumi wa China unatimiza maendeleo yenye ubora wa kiwango cha juu, badala ya kupata ukuaji wa kasi tu.
Amesema kufanikisha mabadiliko hayo ni msingi kwa China kutunga sera zake za kiuchumi, kijamii, kimuundo na za mageuzi kwa miaka kadhaa ijayo, na kwamba wakati China inaendelea kufungua mlango, mabadiliko hayo mapya kwenye maendeleo yake yatatoa fursa kubwa kwa sekta mbalimbali mpya, sio nchini China tu, na bali pia kwa dunia nzima kwa ujumla.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |