• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa misaada ya kibinadamu kwa Somalia

  (GMT+08:00) 2018-01-25 19:45:00

  Hafla ya kukabidhi misaada ya kibinadamu iliyotolewa na China kwa serikali ya Somalia imefanyika jana kwenye bandari ya Mogadishu nchini Somalia.

  Ubalozi wa China nchini Somalia ulieleza kuwa misaada hii ni pamoja na mahema 30,000, vyandarua 10,000 na matanki 500 ya kuhifadhi maji.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Balozi wa China nchini Somalia Bw. Qin Jiang amesema urafiki kati ya China na Somalia ni wa kijadi, na China siku zote inaunga mkono amani na maendeleo ya Somalia na kufuatilia hali ya binadamu nchini Somalia kwa kutoa misaada ya dharura kwa mahitaji ya Somalia. Misaada hiyo ilipelekwa kwa vikundi vitatu na vitawanufaisha watu waliopoteza makazi yao na wanaoathirika na maafa ya ukame nchini Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako