• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka wa sera yake kuhusu Ncha ya kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-01-26 10:49:17

    Ofisi ya habari ya Baraza la serikali la China imetoa waraka wa sera yake kuhusu Ncha ya kaskazini, ikiwa ni mara ya kwanza kwa China kutoa waraka kama huo.

    Waraka huo unasema China inayopendekeza kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, siku zote ni mshiriki, mjenzi na mchangiaji wa shughuli za Ncha ya kaskazini, na inajitahidi kuchangia busara na nguvu ya China kwa ajili ya maendeleo ya Ncha ya kaskazini.

    Waraka pia unasema China ikiwa ni nchi yenye kuwajibika, inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kwenye msingi wa kuheshimiana, kunufaishana na kuhimiza maendeleo endelevu, katika kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko yanayotokea katika Ncha ya kaskazini, kuendeleza na kusimamia kwa pamoja Ncha ya kaskazini, ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na utulivu na maendeleo endelevu ya Ncha ya kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako