• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mizozo na mapigano yatatiza ukuaji wa kilimo Afrika

  (GMT+08:00) 2018-01-28 16:41:50

  Nchi za Afrika zimetakiwa kukabili mizozo na mabadiliko ya tabia nchi ili kushinda vita dhidi ya njaa.

  Kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika unaondelea mjini Addis ababa Ethiopia, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa mwito kwa bara la Afrika kuimarisha amani kama njia muhimu ya kustawisha kilimo.

  Pembezoni mwa mkutano wa 30 wa Umoja wa Afrika, viongozi na wadau wa kilimo na chakula pamoja na maafisa wa Umoja wa mataifa wamekutana kujadili jinsi ya kuangamiza njaa barani Afrika.

  Mkutano wao unafanyika miaka mitano baada ya Umoja wa Afrika kutoa azimio la kuangamiza njaa barani humo ifikapo mwaka wa 2025.

  Ingawaje, huku ikisalia miaka 8 tu kabla ya kufanikisha azimio hilo la mwaka 2013, Afrika bado inaendelea kukabiliawa na uhaba wa chakula kutokana mabadiliko ya hali ya hewa, mizozo na umaskini.

  Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia washirika wa mkutano huu anasema

  "Kilimo na uzalishaji wa mifugo barani Afrika unakabiliwa na hatari, hasa kutokana na mapigano na mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa chakula naumaskini zinahusiana kwa karibu.Ni muhimu kuangazia kwamba wengi wa watu wanaokosa chakula barani Afrika, wako kwenye nchi zinazokumbwa na migogoro Kuwa na kilimo shirikishi na endelevu ni muhimu katika kufikia malengo mawili ya kwanza ya maendeleo endelevu ya kuangamiza njaa na umaskini na pia kusomgesha mbele malengo mengine.Kujitolea kikamilifu kwa serikali za Afrika, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Afrika zinahitajika ili kuendeleza amani, haki za kibinadam maendeleo endelevu kama njia moja ya kupambana na njaa"

  Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO zinaonyesha kuwa katika kanda ya Afrika Mashariki pekee nchi za Sudan Kusini, Kenya, Ethiopia, na Somalia watu milioni 28 wanahitaji misaada ya chakula.

  Kulingana na takwimu hizo za mwaka 2017, zaidi ya watoto milioni moja wanakabiliwa na utapia mlo hali inayotia hofu na masikito.

  FAO inaripoti kwamba watu wanaokosa chakula cha kutosha duniani waliongezeka kwa asilimia 30 kati ya mwaka 1990na mwaka 2016, hali ikiwa mbaya zaidi katika kanda ya Sahel na upembe wa Afrika.

  Lakini hata hivyo nchi za Afrika zimeendelea kuongeza uwekezaji kwenye kilimo na hivyo kupunguza idadi ya watu wasio na chakula.

  Kwa mfano nchini Ethiopia serikali imeongeza bajeti yake kwa wizara ya kilimo na kuboresha sera za sekta hiyo ili kuongeza uzalishaji.

  Hailemariam Desalegn ni Waziri mkuu wa Ethiopia na pia mwenyekiti wa mpango wa kina wa maendeleo ya kilimo barani Afrika (CAADP).

  "Kwa wastani kilimo na sekta husika, vimekuwa na ukuaji wa asilimia asilimia 10 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 15 iliopita. tumekuwa tukitenga zaidi ya asilimia 10 ya bajeti ya kitaifa kwa sekta ya kilimo ambayo ni zaidi ya malemho yaliowekwa na mpango wa kina wa maendeleo ya kilimo barani Afrika (CAADP), Pia tulianzisha mpango wa kufanya kilimo biashara ambao umesaidia kuendesha kilimo cha kisasa kwa njia ya mashine"

  Nchi nyingi barani Afrika hutegemea kilimo kama njia kuu ya kuendeleza uchumi.

  Lakini kutokana na changamoto zinazoathiri uzalishaji endelefu kama kupungua kwa mvua na ukosefu wa mtaji wa kutosha sekta hiyo bado haijakua kikamilifu.

  Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa shirika la kilimo na chakula duniani FAO Jose Graziano da Silva anasema hatua mpya za shirika hilo zitasaidia frika kupiga hatua za kuelekea kujitosheleza na chakula.

  "Uwekezaji katika sekta ya kilimo unasalia kuwa njia bora zaidi ya kuwezesha familia kuwa na mapato na pia lishe bora barani Afrika.Naridhika kusema kwamba tunaingia awamu mpya yenye matumaini ya kuwa na hatua kuwa na hatua bora sekta ya kilimo mwaka huu wa 2018"

  Umoja wa mataifa unapendekeza kuwa serikali za Afrika zinafaa kutenga angalau asilimia 10 ya bajeti yake ya kitaifa kwa sekta ya kilimo.

  Malengo muhimu ya Umoja huo ni kuwa na dunia yenye chakula cha kutosha ifikapo mwaka 2030.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako