• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka-Usajili, Mazungumzo baina ya timu za Dortmund na Arsenal kuhusu uhamisho wa Aubameyang yaelezwa kuendelea vizuri.

    (GMT+08:00) 2018-01-29 09:40:24

    Mazungumzo baina ya Arsenal na Borussia Dortmund yanaelezwa kuendelea vyema na kwamba huenda zikakubaliana juu ya uhamisha wa mchezaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang.

    Imefahamika kuwa Arsenal wamekuwa wakiwinda saini ya mchezaji huyo kwa muda mrefu lakini maombi yao yalikuwa yakikataliwa na Dortmund kwa kuwa hawakufikia vigezo ikiwemo dau la Pauni milioni 60, linalodaiwa kuwa huenda sasa wakatoa, ili kumnyakua kabla dirisha dogo la usajili halijafungwa.

    Wakati huo huo, hatma ya mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ya kuihama klabu hiyo itajulikana endapo suala la Aubameyang likikamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako