• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 30 wa kilele wa Umoja wa Afrika wafunguliwa Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-01-29 10:59:12

    Mkutano wa 30 wa kilele wa Umoja wa Afrika ulifunguliwa jana katika makao makuu ya umoja huo huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia.

    Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Kupata ushindi katika mapambano dhidi ya ufisadi: Njia endelevu kwa Afrika kujiendeleza".

    Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mataifa Bw. Moussa Faki Mahamat anasema, hatua za mageuzi ya umoja wa Afrika zinapaswa kuharakishwa, ili kuongeza uwezo wa umoja huo kufanya mapambano, na kwamba kuharakisha mchakato wa mfungamano wa bara la Afrika ni njia ya lazima kwa maendeleo ya Afrika.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema kwenye mkutano huo kuwa, Umoja wa Mataifa utaimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Afrika katika ulinzi wa amani na usalama, maendeleo endelevu, haki za wanawake na vijana, wahamiaji, na mapambano dhidi ya ufisadi.

    Katibu mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Bw. Ahmed Aboul Gheit amesema, Umoja huo unatarajia kuimarisha ushirikiano kati yake na Umoja wa Afrika katika sekta za amani na usalama.

    Nchi za Afrika zimekubaliana kupigana vita dhidi ya Ufisadi kwa kufunga mianya yote, kuwaadhibu wahusika katika ufisadi na Kufungua taasisi maalum kwa ajili ya kupambana na ufisadi, zote hizi zikiwa ni sehemu ya uzoefu wa njia ambazo nchi za Afrika zimejifunza kutokana na mafanikio ya China katika vita dhidi ya Ufisadi.


    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako