• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wafungwa

    (GMT+08:00) 2018-01-30 09:54:15

    Mkutano wa kilele wa umoja wa Afrika umefungwa jana mjini Addis Ababa na kutoa mwito wa kuhimiza umoja kwenye mapambano dhidi ya ufisadi.

    Mkutano huo uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika, umeeleza umuhimu wa kutokomeza ufisadi na umaskini barani Afrika, pamoja na kuharakisha utekelezaji wa ajenda ya kuelekea mwaka 2063.

    Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika Rais Paul Kagame wa Rwanda, amesema kwenye ufungaji kuwa mkutano huo umepata mafanikio kwenye maamuzi ya mambo makubwa, yanayoweza kulisaidia bara la Afrika kutimiza malengo yake ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ya maendeleo ya Afrika.

    Wakati wa mkutano huo ushirikiano kati ya China na Afrika pia ulitajwa. Kamishna wa mambo ya siasa wa umoja wa Afrika Bw Khabele Molotsa amesema Umoja wa Afrika na China wana uhusiano imara uliojengwa kwa msingi wa kuheshimiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako