• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu Tanzania Bara: Rekodi zawekwa mzunguko wa kwanza ukimalizika

    (GMT+08:00) 2018-01-30 10:55:02

    Nchini Tanzania wakati huu ambapo ligi kuu imemaliza mzunguko wa kwanza, kuna rekodi nyingi zimeandikwa, miongoni mwa rekodi hizo ni pamoja na ya golikipa wa simba sports club Aishi Salum Manula ambaye katika mechi 20 alizodaka tangu ajiunge na Simba SC hajaruhusu kufungwa goli katika mechi 14.

    Katika mechi sita ambazo aliruhusu goli langoni kwake msimu huu hakuna hata mechi moja ambayo Simba ilifungwa katika dakika tisini za kawaida, nyingi ziliisha kwa simba kushinda na zingine sare ya magoli.

    Rekodi yake hiyo imeisaidia timu yake ya Simba kumaliza duru la kwanza la mzunguko wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 15, zikiwa ni pointi saba zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga walioko nafasi ya tatu na pointi tano, zaidi ya Azam FC wanaoshika nafasi ya pili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako