• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuuhimiza Umoja wa Mataifa utoe mchango mkubwa zaidi katika kulinda amani ya dunia

    (GMT+08:00) 2018-02-01 09:31:43

    Balozi mpya wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Ma Chaoxu amesema, China itashirikiana na jumuiya ya kimataifa kuuhimiza Umoja wa Mataifa utoe mchango zaidi katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

    Bw. Ma Chaoxu aliyasema hayo alipokabidhi hati za utambulisho kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres mjini New York. Amesema China itatoa mchango katika kuhimiza ujenzi wa uhusiano mpya wa kimataifa wa kuheshimiana, wenye haki na usawa na ushirikiano wa kunufaishana, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Pia amesema China ikiwa ni mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa na nchi kubwa inayowajibika, italinda kithabiti mamlaka na hadhi ya Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi muhimu kwenye jukwaa la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako