• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Uingereza wakutana Beijing

    (GMT+08:00) 2018-02-01 10:15:26

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alasiri hapa Beijing amekutana na mwenzake wa Uingereza Bi. Theresa May ambaye yuko ziarani nchini China.

    Kwenye mazungumzo yao, Bw. Li Keqiang amesema China siku zote inatilia maanani Uingereza na uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na inaamini kuwa kudumisha maendeleo tulivu ya uhusiano huo kunalingana na maslahi ya pamoja ya pande mbili, na pia kunasaidia kuhimiza amani, utulivu na ustawi wa kikanda na duniani.

    Kwa upande wake Bi. Theresa May amesema anapenda kutumia fursa ya ziara yake kukuza zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya Uingereza na China, na pia Uingereza inapenda kushirikiana na China kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda mmoja njia moja", na kutafuta ushirikiano kati ya nchi mbili kwenye nyanja za uvumbuzi, fedha, kulinda hakimiliki na teknolojia ya akili bandia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako