• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Kombe la Mashujaa-Rwanda: Wapinzani wa jadi APR na Rayon Sport kucheza leo mjini Kigali.

    (GMT+08:00) 2018-02-01 14:38:09

    APR wapo katika mtihani mzito leo, watakapocheza na WAPINZANI wa jadi katika historia ya soka la Rwanda Rayon Sport katika uwanja wa Amahoro, kwenye mechi ambayo inaweza kuamua bingwa wa mashindano ya kombe la Mashujaa.

    APR ambao ndiyo mabingwa watetezi, wanapointi moja tu katika mechi mbili walizocheza, wakiwa wametoka sare katika mechi moja dhidi ya AS Kigali, na wakiwa wamefungwa mechi nyingine dhidi ya Polisi. Hivyo ushindi katika mechi ya mwisho leo unaweza kuleta matumaini ya ubingwa.

    Kikwazo ni kwamba, hata kama wakishinda mechi hiyo, kikwazo kitakuwa ni mechi nyingine ya kombe hilo itakayopigwa leo, baina ya Polisi wenye pointi 3 na AS Kigali wenye pointi 2, na endapo Polisi endapo yeyote atashinda mechi hiyo, ARP hawatakuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa.

    Kwa upande wao Rayon wenye pointi 4, ushindi tu, moja kwa moja unawapa ubingwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako