• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Uingereza wazungumza na wajasiriamali kutoka nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-02-01 17:46:17

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May ambaye yuko ziarani nchini China wamehudhuria hafla ya kuanzisha Kamati ya Wajasiriamali kutoka China na Uingereza na kuzungumza na wajumbe wao.

    Bw. Li Keqiang amesema, hivi sasa uchumi wa dunia unafufuka, kuanzishwa kwa Kamati hiyo kutaimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bi. May amesema, baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, Uingereza itaendelea kufungua mlango, na Uingereza na China zinatarajiwa kuanzisha uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi na kibiashara.

    Wajasirimali kutoka kampuni zaidi ya 30 za nchi hizo mbili zinazojikita katika mambo ya fedha, nishati, mawasiliano ya simu, magari, dawa na usafiri wamefanya majadiliano ya kina kuhusu masuala ya biashara, uwekezaji, soko huria, na ushirikiano wa uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako