• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Hazina ya fedha yalenga kukusanya franki trilioni 1.2

    (GMT+08:00) 2018-02-01 20:01:51

    Halmashauri ya ushuru nchini Rwanda RRA inalenga kukusanya franki trilioni 1.2 kama ushuru kufikia mwezi juni mwaka huu.

    Katika kipindi cha nusu ya mwaka jana,halmashauri hiyo ilikusanya franki bilioni 582.7 ambayo ni zaidi ya asilimia 10 ya mwaka uliopita.

    Sekta za miundo msingi,bidhaa kutoka nje,uchimbaji madini zinatarajiwa kuingiza fedha zaidi.

    Ikiwa moja ya nchi zinakua kwa kasi katika masuala ya kiuchumi ,Kamishena mkuu wa halmashauri hiyo,Richard Tusabe analenga ukuwaji wa zaidi ya asilimia 7 ya uchumi katika nchi hiyo.

    Rwanda inajikakamua kufikisha franki bilioni 10 mwa miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu.

    Hatua hii inawezekana kufuatia kuanzishwa kwa mbinu za ulipaji ushuru za dijitali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako