• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Balala akataa kupinga marufuku ya shisha

    (GMT+08:00) 2018-02-01 20:02:08

    Waziri wa utalii nchini Kenya Najib Balala amekataa kupinga marufuku ya shisha .

    Akiongea na wanahabari,balala amesema anaunga kikamilifu marufuku hayo lakini ameitisha mda kwa washikadau wajitayarishe.

    Marufuku hiyo ya ghafla iliathiri hoteli za kitalii kwani hakukuwa na ilani .

    Balala amesema ni vyema kwa serikali kuwaarifu wadau haswa wanaotoa huduma za kitalii kuhusu swala ambalo ni tofauti na sheria za baadhi ya nchi.

    Shisha ilipigwa marufuku nchini Kenya baada ya onyo kutoka kwa shirika la afya duniani kuhusu madhara yake .

    Kulingana na Balala huenda kungeweka udhibiti wa uvutaji wa shisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako