• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping akutana na waziri mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May

    (GMT+08:00) 2018-02-02 09:30:20

    Rais Xi Jinping wa China amekutana hapa Beijing na waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May anayefanya ziara nchini China. na kufanya naye mazungumzo kuhusu namna ya kuhimiza zama nzuri ya uhusiano kati ya China na Uingereza.

    Rais Xi amesema amani, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana vimekuwa ni mkondo mkuu kwenye maendeleo ya dunia yenye ncha nyingi, mafungamano ya kiuchumi, uwepo wa tamaduni mbalimbali na matumizi makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

    Rais Xi amemwambia Bibi May kuwa China na Uingereza zinatakiwa kuendana na mwelekeo wa sasa, kuitikia mahitaji ya maendeleo ya kila upande na kuongeza mambo mapya kwenye zama nzuri ya uhusiano kati ya nchi zao.

    China na Uingereza zilikaribisha zama nzuri ya uhusiano kati yao baada ya Rais Xi Jinping kufanya ziara nchini Uingereza mwaka 2015.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako