• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana Tanzania kufundishwa jinsi ya kuhudumia SGR

    (GMT+08:00) 2018-02-02 19:53:36

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Masanja Kadogosa, kutayarisha timu ya vijana kuwafundisha kwa ajili ya kuhudumia reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) itakapokamilika.

    Profesa Mabarawa alitoa agizo hilo wakati alipotembelea mradi huo kutoka Soga Kibaha mkoani Pwani hadi Pugu jijini Dar es Salaam, ili kujionea maendeleo ya mradi huo unaotarajiwa kukamilika Juni 2020 huku awamu ya kwanza ikiwa tayari imeanzwa kutekelezwa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa urefu wa kilometa 300.

    Alisema suala la kuwafundisha vijana kwa ajili ya kuhudumia reli hiyo lipo kwenye mkataba kati ya Rahco na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki inayojenga reli hiyo hivyo ni vyema wakaandaa vijana sasa kwa ajili ya kuwapeleka kwenye mafunzo ili reli hiyo itakapoanza kazi iendeshwe na Watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako