• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Areruya ashinda ubingwa mwingine wa Afrika, na kuisaidia Rwanda kufuzu mashindano ya dunia

    (GMT+08:00) 2018-02-05 08:43:06

    Kwa mara nyingine tena Joseph Areruya amewika baada ya kutwaa taji ligine la kimataifa la mashindano ya baiskeli alipotangazwa kuwa mshindi wa mbio za vijana chini ya Umri wa miaka 23 zilizomalizika jana nchini Cameroun.

    Areruya aliibuka mshindi baada ya kutumia saa 10 dakika 27 na sekunde 34 katika umbali wa kilomita 417 kuanzia mjini Douala hadi mji wa Younde.

    Ushindi wa Areruya umempa nafasi yeye pamoja na timu ya taifa ya Rwanda kushiriki mashindano ya Ufaransa yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

    Na baada ya kukamilika kwa mashindano hayo, Areruya na timu yake ya Rwanda sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mashindano mengine ya Afrika yatakayofanyika nchini Rwanda kuanzia jumanne ya wiki ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako