• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Morocco ndiyo mabingwa wapya wa mashindano wa CHAN

  (GMT+08:00) 2018-02-05 09:04:16

  Morocco ndiyo mabingwa wapya wa mashindano ya soka ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani kufuatia ushindi waliopata jana kwenye mechi ya fainali walicheza dhidi Nigeria.

  Morocco walishinda kwa magoli 4-0 yaliyofungwa na Zakaria Hadraf aliyefunga mawili, dakika ya 45 na 64, Walid El Karti dakika ya 61 na Ayoub El Kaabi dakika 73, ambaye pia aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kufunga magoli 9, pia kutaokana na umahiri wake alitangazwa mchezaji bora wa mashindano.

  Kwa ushindi huo, Morocco ambao walikuwa wenyeji wa mashindano hayo wamejinyakulia kombe, medali za dhahabu na fedha taslimu dola za kimarekani milioni 2.5

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako