• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yatangaza kurejea kwenye Jumuiya ya Madola mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-02-05 09:07:23

    Gazeti la The Sunday Mail la Zimbabwe limeripoti kuwa, rais Emmerson Mnangagwa wa nchi hiyo amewasilisha nia ya Zimbabwe kurejea kwenye Jumuiya ya Madola mwaka huu kwa serikali ya Uingereza.

    Gazeti hilo limesema, rais Mnangagwa ameeleza wazi msimamo huo wakati wa mazungumzo kati yake na mjumbe maalumu wa serikali ya Uingereza ambaye pia ni waziri mpya wa mambo ya Afrika wa Uingereza Bi. Harriet Baldwin.

    Ripoti hiyo imewanukuu maofisa wa Zimbabwe walioshuhudia mazungumzo hayo wakisema kuwa, rais Mnangagwa pia amesisitiza kuwa Zimbabwe haitabadilisha msimamo wake wa kufanya mageuzi kuhusu suala la ardhi, na kwamba serikali ya Uingereza inapaswa kubeba wajibu wake wa kutoa fidia kwa wazungu waliokuwa na mashamba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako