• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa waraka unaoelekeza mkakati wa ustawi vijijini

  (GMT+08:00) 2018-02-05 16:21:51

  Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kwa kushirikiana na Baraza la Serikali imetoa waraka wa kwanza wa mwaka 2018 unaoelekeza utekelezaji wa mkakati wa kustawisha maeneo ya vijijini.

  Waraka huo umeeleza mustakabali wa sera za kuongeza kasi ya kujenga kilimo na vijiji kuwa ya kisasa na kuchukua njia ya kustawisha vijiji ya ujamaa wenye umaalum wa kichina. Waraka huo umesema, kutekeleza mkakati wa kustawisha maeneo ya vijijini ni matakwa ya lazima ya kutatua mgongano kati ya mahitaji ya wananchi yanayoongezeka siku hadi siku ya kutafuta maisha bora na maendeleo yasiyo na uwiano, pia ni matakwa ya lazima ya kutimiza utajiri wa wananchi wote.

  Kwa mujibu wa waraka huo, pamoja na mambo mengine, China itainua ubora wa maendeleo ya kilimo, kuhimiza maendeleo vijijini yasiyo na uchafuzi, kustawisha utamaduni wa vijijini, kujenga utaratibu mpya wa usimamizi wa maeneo ya vijijini, na kuinua kiwango cha uhakikisho wa maisha ya wakazi wa maeneo ya vijijini.

  Profesa Qin Fu wa Taasisi ya Sayansi Kilimo ya China amesema, China imepata mafanikio mfululizo katika sekta ya kilimo na ujenzi wa maeneo ya vijiji, lakini bado kuna mengi ya kufanywa ili kushughulikia matatizo kama vile ubora usioridhisha wa maendeleo ya kilimo na pengo kubwa kati ya pato la wakulima na wakazi wa mijini. Anasema,

  "Kwa kupitia uingiliaji wa serikali na usimamizi wa jumla, mambo ya kilimo, vijiji na wakulima yanaweza kuendelezwa kwenye ngazi ya juu zaidi, pia kunaweza kuwa injini mpya kwa maendeleo ya kilimo na vijiji katika siku za baadaye, na kuinua nguvu ya ushindani."

  Naye profesa Zhang Qi wa Chuo Kikuu cha Ualimu cha Beijing anaona kuwa, kabla ya mwaka 2020, kazi ya kuondoa umaskini ni jukumu kuu katika mkakati wa kustawisha maeneo ya vijijini nchini China, pia ni nyongeza muhimu ya kutimiza maendeleo yasiyochafua mazingira vijijini na kuinua ubora wa maendeleo ya kilimo. Anasema,

  "Baada ya mwaka 2020, suala la umaskini wa kulinganishwa linaweza kuathiri kasi ya maendeleo ya kustawisha maeneo ya vijijini na matokeo yake. Lakini hivi sasa umaskini unaokithiri ni sababu kuu, tunajitahidi kuondoa umaskini unaokithiri, na maeneo yasiyo na umaskini unaokithiri yanapaswa kuanza kutatua umaskini wa kulinganishwa. Aidha, kupunguza umaskini kwa kujihusisha na shughuli zisizochafua mazingira na zinazotegemea maumbile ya asili ni njia endelevu zaidi ya kupunguza umasikini."

  Wakati huohuo, mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa kazi ya vijiji cha serikali kuu ya China Bw. Han Jun amesema, mkakati wa kustawisha vijiji ni mkakati mkubwa wa chama na taifa, ambao pia ni jukumu la kihistoria litakalodumu kwa muda mrefu. Pia amesisitiza kuwa mkakati huo unazingatia sana utekelezaji, ambao unahitaji uwekezaji halisi na mazingira bora yenye sera kamili zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako