• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yafanyika upya huko Addis Ababa

  (GMT+08:00) 2018-02-06 08:36:14

  Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD imeanzisha tena mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini jana huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ambayo yametishia kuchukua hatua za kuadhibu pande mbalimbali zinazopambana.

  Mkutano huo unaoitwa Kipindi cha pili cha Baraza la ngazi ya juu la ustawi umefanyika baada ya kusainiwa kwa Makubaliano ya kusitisha mapambano tarehe 24 Desemba mwaka 2017, ambayo yalivunjika saa chache baada ya kuanza utekelezaji wake.

  Mjumbe maalumu wa IGAD kwenye suala la Sudan Kusini Bw. Ismael Wais amezitaka pande mbili zinazopambana zisitishe mapambano, ili kuweka na kuimarisha mafanikio, uaminifu na imani zilizoanzishwa na Makubaliano ya kusitisha mapambano. Amesema Umoja wa Afrika, IGAD, Umoja wa Mataifa, pamoja na jumuiya ya kimataifa zimetoa taarifa kali za kulaani ukiukaji wa Makubaliano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako