• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho la mchezo wa mbio za baiskeli laipongeza timu ya taifa kwa ushindi wa Cameroun

    (GMT+08:00) 2018-02-06 09:07:44

    Chama cha Mchezo wa Baiskeli nchini Rwanda FERWACY kimeipongeza timu ya taifa kwa mafanikio iliyopata kwenye mashindano ya mataifa ya Afrika yaliyomalizika nchini Cameroun ikiwa ni baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa na kufuzu mashindano ya dunia mwezi Agosti nchini Ufaransa.

    Akitoa pongezi hizo, kipekee Rais wa FERWACY Aimable Bayingana amemsifu Joseph Areruya kwa kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya taifa kimataifa kwenye mchezo huo, lakini pia kwa kuendelea kuiongoza vyema timu ya taifa.

    Rais huyo amesema licha ya ushindi huo, timu hiyo haitakuwa na nafasi ya kupumzika, hivyo moja kwa moja itakwenda kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mengine ya bara yatakayofanyika mjini Kigali kuanzia tarehe 12 ya mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako