• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Magedo yakosesha serikali ya Kenya ushuru wa ngozi

    (GMT+08:00) 2018-02-06 18:44:17

    Magedo kwenye sekta ya ngozi nchini Kenya yametajwa kama mojawepo wa changamoto kubwa zinazoathiri sekta hiyo.

    Chama cha wenye viwanda vya ngozi kimesema kila mwaka jumuiya ya Afrika mashariki inapoteza hadi dola milioni 30 kutokana na ukwepaji wa kulipa kodi za ngozi.

    Mkurugenzi wa mamlaka ya maendeleo ya ngozi nchini Kenya Dkt. Issack Noor amesema bado hakuna sheria ya kutouza nje ngozi ghafi lakini imeongeza ushuru unaotozwa wauzaji kutoka asilimia 40 hadi asilimia 80 ili kuwahimiza wadau kuongeza ubora kabla ya kuuza nje.

    Lakini hata hivyo amesema ushuru huo wa juu umefungua mianya ya magedo na hivyo kuikosesha serikali mapato.

    Kulingana na bajeti ya mwaka 2018, Kenya inalenga kuongeza asilimia 15 ya utengenezaji bidhaa na sekta ya ngozi ni mojawepo wa zile zinazopangiwa kupanuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako