• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan Kusini yapinga Marekani kuiwekea vikwazo vya kuuziwa silaha

  (GMT+08:00) 2018-02-07 09:42:13

  Maelfu ya raia wa Sudan Kusini jana walifanya maandamano huko Juba, mji mkuu wa nchi hiyo, wakiipinga Marekani kuiwekea nchi yao vikwazo vya kuuziwa silaha kutokana na pande zinazopambana nchini humo kushindwa kufuata makubaliano ya kusimamisha vita.

  Waandamanaji hao walikuwa wakielekea ubalozi wa Marekani na makao makuu ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS ambako waliwasilisha malalamiko yao. Kwenye malalamiko hayo, viongozi wa waandamanaji wamelaani hatua hiyo ya Marekani na kudai itadhoofisha uhuru wa nchi hiyo waliopigania na kukwamisha mchakato wa kupata ustawi.

  Ijumaa iliyopita, serikali ya Marekani ilitangaza kuiwekea Sudan Kusini vikwazo, na kulihimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza zuio la kusafirisha silaha dhidi ya Sudan Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako